Wednesday, January 5, 2011
PANDE ZANGU BY KHADIL
Helo ni mara nyingine wapenzi wa blog hii tunakutana nashukulu kuona mnaniunga mkono sasa kwakuwa mmekuwa nami bac jiandae kwa makala mpya inayokuja inayohusu wachumba nadhani hili litakuwa darasa tosha kwa wachumba.Hakika najiandaa kuwaelimisha kwa udi na vumba sio kwamba nawaelimisha bali tunaelimishana
Monday, January 3, 2011
KONA YA MMILIKI WA WEBSITE HII BY KHADIL
JAMANI MUOKOE MWENZI WAKO IKIWA ANATOA HARUFU MBYA BY KHADIL
Jambo la kwanza unapoanza kusoma safu hii ni kumshukuru Mungu kwa kukuwezesha kufika leo, ikiwa ni siku ya tatu ya mwaka mpya wa 2011. Wema wake ni mkubwa mno kwako ndiyo maana amekubakiza, kwa hiyo ni deni kwako kuulipa.
Ilikuwa mbaya kwa wale waliopata misukosuko ya hapa na pale. Inauma kumpoteza yule uliyempenda iwe kwa ugomvi, kifo au sababu yoyote ile. Natumia fursa hii kutoa pole kwa kila aliyefikwa na baya lolote mwaka 2010.
Turudi kwenye mada yetu, leo ikiwa ni sehemu ya nne. Wiki iliyopita niliandika namna yas kushughulikia nywele za kwapa pamoja na zile nyeti. Bila shaka utakuwa umepata kitu cha kuzingatia katika kuboresha uhusiano wako.
HARUFU
Msomaji utakuwa shahidi kuhusu hili kwamba tatizo la harufu ya mwili hasa maeneo nyeti, ni kitu ambacho kinawaaibisha wengi. Wake kwa waume wanaumbuliwa na hili. Kama hujaona, basi umesikia au kusimuliwa.
Watu wengi hawana simile, wasipowaeleza wenzi wao kuhusu kero ya harufu, basi watakwenda kuyazungumza mitaani kwa marafiki. Wote hao wana kasoro ya kutojua maana ya mapenzi na wajibu wao.
Rafiki yangu mmoja aliwahi kunisimulia namna alivyomfukuza mpenzi wake wa ‘kula na kuondoka’ chumbani gesti baada ya kumbaini anatoa harufu mbaya, hasa sehemu nyeti. Alisukumwa zaidi na ujana.
Aliniambia: “Justina ni mzuri tu kwa juu, nimeingia naye chumbani duh! Nilishindwa kuvumilia harufu, nikamtimua chumbani.” Ni uamuzi wake lakini iliniuma mno.
Niliwaza sana kuhusu namna yule dada alivyoumia. Ni mrembo lakini alitendwa na kijana ambaye alikosa uungwana. Si kila ukweli unafaa. Unatakiwa uwe sahihi mdomoni lakini siyo kung’ang’aniza ukweli wako.
Hapa namaanisha kuwa unaweza kusema ukweli lakini ukakosa uungwana. Mfano hai ni huyo rafiki yangu. Inawezekana ni kweli huyo mpenzi wake anatoa harufu iliyomkera ila alipungukiwa busara katika kumfikishia ujumbe.
Stori nyingine ni tukio ambalo nililishuhudia kwa macho yangu. Siku moja nilikwenda kumtembelea rafiki yangu lakini kilichotokea ni kama ule msemo wa “ukitembea uchi ndiyo unakutana na mkwe barabarani.”
Huyo rafiki yangu akavua viatu, mkewe bila hata kunionea aibu mimi mgeni, akamrudi mumewe. Akamwambia: “Aah … (alitaja jina la rafiki yangu), miguu yako inanuka bwana, hizo soksi hufui? Unatuchafulia hali ya hewa.”
Kauli hiyo ilimnyong’onyeza rafiki yangu, akawa mpole. Aliniangalia kwa jicho lenye kusema: “Naomba uyavumilie ya nyumba hii.” Kimsingi mke wa ndugu yangu hajastaarabika hata kidogo.
Sikupata picha ni nini alichofundishwa kwenye ‘kitchen party’. Mwanamke mstaarabu hawezi kuwa mropokaji kwa kiwango hicho. Alichosema ni kweli lakini alivyofikisha ujumbe haikuwa sahihi.
UNAWEZA KUEPUKA FEDHEHA!
Muhimu ni wewe kujitunza kwanza kabla hujaumbuliwa. Jifanyie usafi na uhakikishe unakuwa mfano bora kwa wengine. Iwe ni mwanamke au mwanaume unaweza, kimsingi ni dhamira yako ndiyo inayokutuma.
Hata kama nafundisha mwenzi wako asikuchakachue unapotoa harufu mbaya, kilicho bora ni wewe kuheshimu utu wako kwa kujiweka nadhifu. Mwenzio anapokukuta msafi, unajiongezea alama za kupendwa.
MWENZI ANANUKA, DAWA NI HII
Usithubutu kumuanika mwenzi wako kwa ubaya. Jaribu kumueleza yeye kwa nafasi yake mkiwa wawili, tena kwa lugha laini ili aweze kukuelewa. Penda kufundisha badala ya kutoa matamshi ya kuudhi.
Fundisha kwa kuonesha mfano, kama soksi zake zinatoa harufu, hupaswi kumnanga mbele za wageni. Shughulikia kwa namna bora kabisa. Wewe ni mwanamke, mfulie kwani usipofanya hivyo mwisho ni aibu yenu wote.
Kwa kawaida wewe unapochekesha, jamii humtazama zaidi mwenzi wako. Mathalani unavaa nguo chafu au umezunguka mtaani uchi, aibu itakuwa kwa mwandani wako kwa maana kila mtu atamsema kwako. Mke wa fulani au mume wa fulani.
Mkeo mvivu anashindwa kufanya usafi, nawe upo ‘bize’, kilichopo mbele yako ni kuajiri mfanyakazi ili akuepushie aibu. Ashughulikie usafi wa kuonekana ili wewe uanze kudili na ule wa faragha.
HARUFU YA FARAGHA
Umehakikisha kila kitu kipo kwenye mstari lakini bado mwenzi wako anatoa harufu inayokera hasa eneo nyeti. Bila shaka unapata kinyaa kuendelea naye lakini hapo siyo mwisho. Kuna kitu cha kufanya zaidi.
Itaendelea wiki ijayo...KHADIL KANTANGAYO

Saturday, January 1, 2011
KONA ZA WCHUMBA
2011 uyamiliki mapenzi, yakikumiliki utalia wiki 52

Kinyume chake ni kilio cha mwaka mzima. Mada hii itakuwa na lengo moja tu la kuwaponya wale wote wanaoishi kwenye mapenzi yasiyo na amani. Yale yanayoashiria kifo cha mapema na kuwafanya wabadili uelekeo.
Wanaweza kuanza kuheshimu kile kilichowaunganisha. Yaani kuufanya ‘uspesho’ wao uwe na maana. Ikiwa hivyo, basi watakuwa wanaondokana na jinamizi la kifo cha haraka. Hapa si utani, inahitaji utulivu kujua.
Msongo wa mawazo kila siku au mara kwa mara, husababisha mwili kushindwa kufanya kazi sawasawa. Athari kubwa huelekea kwenye moyo ambao ndiyo injini ya mwili wa binadamu.
Mapenzi ndiyo kitu namba moja kinachoweza kumfanya mtu awe na msongo mkubwa wa mawazo. Pesa au njia za pesa, ni kichocheo namba mbili lakini kina unafuu wake pale unapopata faraja kutoka kwa mwenzio.
Katika mapenzi, hakuna kinachoweza kukupa ahueni zaidi ya kuelewana na yule unayempenda hata kama amekuudhi, vinginevyo utakosa utulivu wako. Mapenzi yanaua lakini sizungumzii kunywa sumu.
Nazungumzia athari inayojengeka katika moyo baada ya kutokuwa kwenye maelewano chanya na mwenzi wako. Mwili unakosa upumuaji mzuri, hivyo kutema sumu ndani kwa ndani. Matokeo yake unajiona mgonjwa kumbe mapenzi.
NALIGUSA KUNDI HILI
Mtu hana maelewano na mwenzi wake, moyo unamlazimisha atafute suluhu lakini anakuwa mbishi. Anataka kujionesha kwamba yeye yupo salama na hatishiki kwa lolote.
Saikolojia inakutaka ujitunze usiumizwe. Yaani uwe na tahadhari kutafuta suluhu pale isipostahili lakini kama ishu ni ndogo, iweje isiwekwe mezani na kutafuta ufumbuzi?
Mara nyingi mtu huyu huumia sana baadaye hasa baada ya kugundua ukweli kuwa yule aliyekuwa anamfanyia ‘ushenzi’ ameshaondoka na pengine hatarudi tena kwake. Amechezea mawe, kapoteza almasi lakini majuto mjukuu!
HILI NALO LIMO
Ipo jamii ya watu ambao hutaka jamii iwaone wao ni ngangari katika mapenzi. Yaani hawawezi kuumia hata wafanywe nini. Wanajidanganya kwa ‘ubishoo’ wao. Kuna kitu utajifunza leo.
Ukweli ni kuwa hakuna mtu ambaye anaweza kujitenga na maumivu ya moyo pale anapoumizwa na mtu anayempenda. Anaweza kutabasamu akiwa na wewe lakini peke yake ni kilio cha ndani kwa ndani.
Yaani hayupo kwenye hali nzuri na mwenzi wake lakini eti anadhani akisema atachekwa. Ameshajiaminisha yeye ni ngangari lakini ikae kichwani kuwa mtu wa aina hii ni rahisi kufa.
Si kwa kujinyonga isipokuwa anaweza kuangamia taratibu. Hapa nataka nikupe pointi bora ya maisha kuwa; Fanya kila uwezalo kuhakikisha moyo wako unakuwa salama. Usiupe mzigo usio wa lazima.
Maumivu ya mara kwa mara ya kimapenzi ni mzigo mkubwa mno ambao huutwisha moyo wako. Masikini ya Mungu, wenyewe huwa hausemi kwa kutoa sauti ila unapoelemewa maumivu hukurudia mwenyewe.
USILISAHAU NA HILI
Wapo ambao huumizwa wao lakini kutwa kiguu na njia kutafuta suluhu. Haikatazwi kwa maana anatafuta amani ya moyo wake lakini muhimu ni je, huyo anayehangaikiwa yuko vipi?
Ni kujipa mzigo mzito kichwani kubembeleza penzi la mtu ambaye hana hisia na wewe hata kidogo. Bora uumie leo, tafuta faraja kwa watu wako wa karibu, omba kwa Mungu akuvushe salama katika kipindi kigumu.
Anakutenda leo, wewe ndiye unayepigana kutafuta amani irejee na upendo uendelee. Binadamu alivyo na hulka ya ajabu, ukifanya hivyo hawezi kukuona ni mtu bora, isipokuwa ataamini amekupata na huna ujanja, hivyo atarudia yale yale.
DAR HUYU NDO MFALME
NAKUBALI ETO'O ANASTAHILI UFALME WA SOKA AFRICA...

Kwangu mimi ni mmoja kati washambuliaji Hatari zaidi Duniani hasa anapolikaribia goli. Huyo ndio SAMUEL ETO'O FILLS wa Cameroon ambaye juzi aliweka Historia ya kuwa Mwanasoka pekee barani Africa kuweza kutwaa tuzo ya Mwanasoka bora barani humu kwa mara ya 4, maana kina GEORGE WEAH wa Liberia, ABEDI PELLE wa Ghana wamechukua mara 3 na ALHADJI DIOUF wa Senegal amechukua mara 2! ETO'O aliwapiku DIDIER DROGBA wa Ivory coast na ASAMOAH GYAN wa Ghana kwenye kuwania tuzo iyo. Ila najiuliza ivi ni kweli ETO'O ana miaka 29 na Drogba ana 32 kama inavyoelezwa au ni 'kanjanja' 2! Ebu fikiria eti NWANKO KANU ana miaka 34, wakati nimeanza kumsikia KANU tangu nasoma msingi na hata ukimwangalia usoni 2 utajua ana miaka zaidi ya 40 na kitu ivi daah, ama kweli Waafrica kwa mipango bwana...
Pos
UPANDE WA SERIKALI
KUAPISHWA SIO HOJA ILA TUNATAKA UWAZI WA HAKI ZA KISHERIA UPATIKANE...
JK amteua Chande Othman kuwa Jaji mkuu mpya | Send to a friend |
![]() RAIS Jakaya Kikwete, amemteua Jaji Mohamed Chande Othman, kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.Jaji Othman, anachukua nafasi ya Jaji Augustino Ramadhan anayestaafu leo kwa mujibu wa sheria. Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, ilisema Jaji Othman ataapishwa leo Ikulu na ataanza rasmi kazi kesho. "Jaji Othman ataapishwa kesho (leo) saa 4:00 asubuhi, Ikulu jijini Dar es Salaam," ilisema sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mwandishi Msaidizi wa Rais, Premy Kibanga. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Othman alikuwa ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania Jaji huyo pia amewahi kufanya kazi katika nafasi mbalimbali za kitaifa na kimataifa ikiwa ni pamoja na kuwa Makamu wa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Rwanda, iliyoko jijini Arusha. Pia amewahi kushika nafasi sawa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko Timor Mashariki katika kipindi cha kati ya mwaka 2000 na mwaka 2001. Halika kadhalika, amewahi kufanya kazi katika Shirika la Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na Chama cha Msalaba Mwekundu. Mwaka 2006 Jaji Othman, alikuwa ni mmoja wa makamishna wa Baraza la Haki za Binadamu nchini Lebanon kufuatia mgogoro kati ya Lebanoni na Israel. Novemba mosi mwaka 2009, Jaji Othman aliteuliwa kuwa mtaalamu binafsi juu ya hali ya Haki za Binadamu Kusini mwa Sudan, jukumu ambalo atalishikilia hadi Agosti mwakani. Jaji Othman alizaliwa Januari mosi mwaka 1952 na alipata Shahada ya Kwanza ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shahada ya Uzamili (MA) katika Chuo Kikuu cha Webster, Geneva-Uswisi. Jaji Othman anakuwa Jaji mkuu wa tano mzalendo. Jaji wa kwanza mzalendo nchini alikuwa Jaji Agustine Said aliyekuwa anatambuliwa kama Baba wa Mahakama. Jaji Saidi alifuatiwa na Jaji Francis Nyalali na Jaji Barnabas Samatta alikuwa Jaji Mkuu wa tatu akifuatiwa na Augustino Ramadhan, ambaye amemwachia Jaji Othman mikoba hiyo. Juzi Jaji Ramadhan alitoa ushauri kwa mrithi wake kwamba anapaswa kujipanga ipasavyo ili matatizo mbalimbali za Idara ya Mahakama. Akizungumza katika sherehe za kumuaga iliyoandaliwa na Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Jaji Ramadhan alisema kuna mgawanyiko mkubwa katika muhimili huo wa serikali na kwamba hali hiyo ni hatari katika utoaji wa hukumu za haki. Akielezea uzoefu wake wa miaka mitatu na nusu kama Jaji Mkuu wa Tanzania, alisema kuendelea kuwepo kwa makundi miongoni mwa majaji, kunazidisha uwezekano wa kutotenda haki. "Kuna baadhi ya majaji katika vyombo vya sheria ambao kati yao, kuna wanaojiona kuwa wako juu kuliko wengine na hivyo hawapendi kushirikiana na wenzao ambao bado si wazoefu, achilia mbali jamii ambayo wanaitumikia," alisema Jaji Ramadhan. Alisema nafasi ya Jaji mkuu ni kubwa na ndio sura ya chombo cha sheria ambacho majaji waliochini yake, wanapaswa kuiga mifano yake. Jaji Ramadhan ambaye alijielezea kama mtu anayemwogopa Mungu, alisema katika kipindi chote cha uongozi wake aliweza kujichanganya na watu wa kila aina, jambo lililomfanya agundue kuwa kuna baadhi ya majaji nchini hawatendi haki katika hukumu wanazotoa. Alisema kuna kipindi alilazimika kuingilia kati hukumu za kesi mbili ambazo kwa mujibu wa Jaji Ramadhan, hazikuamuliwa kwa haki na kwamba hukumu hizo zilitolewa kwa ajili ya kulinufaisha kundi la watu fulani. Jaji Ramadhan aliweka wazi kuwa kuna madudu mengi yanayofanyika kwenye Mahakama ya Rufaa kwani baadhi ya ushahidi unaotolewa huwa ni wa kupikwa na kwamba ni jukumu la Jaji mkuu kuingilia kati kila mara hali hiyo inapotokea. Jaji Mkuu huyo alikumbushia tukio lililotokea wakati walipokuwa katika kikao kilichowakutanisha majaji wote wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa na kuelezea mtafaruku wa kurushiana maneno ulivyozuka baina ya jaji mmoja wa Mahakama Kuu na mwingine wa Mahakama ya Rufaa. Alisema pia kuna ushirikiano mdogo miongoni mwa majaji katika mahakama hizo kubwa hapa nchini na kuelezea mfano wake alipokuwa akifanya kazi katika Mahakama ya Rufaa. "Kama Jaji wa Mahakama ya Rufaa, baada ya kuandika hukumu nilitakiwa kuigawa pia kwa wenzangu wawili waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo, lakini jaji mmoja alichelewa kuchukua nakala ya hukumu hiyo, na hata alipokumbushwa alionyesha kutokujali," alisema Jaji Ramadhani na kuongeza kuwa ilimbidi aipeleke nakala hiyo kwa Katibu wa Jaji huyo. "Kama kunakuwa na hali hiyo ya kukosa ushirikiano miongoni Mwa wafanyakazi wa mahakama, unadhani haki itatendeka kirahisi," alihoji Jaji Ramadhani na kutoa wito kwa atakayeshika nafasi yake, kulishughulikia jambo hilo. Alisema ofisi ya Jaji mkuu lazima iwe wazi muda wote na iwe inayofikika kirahisi na wananchi kwani kumekuwa na matukio mengi ya ukiukwaji wa haki katika chombo hicho. Jaji huyo anayemaliza muda wake alisema katika kipindi cha uongozi wake, kwa kiasi kikubwa amefanikisha kuboresha uhusiano kati ya serikali, bunge na mahakama kwa sababu mihimili inapaswa kufanya kazi kwa pamoja kwa maendeleo ya nchi. Alifafanua kuwa ili kuhakikisha uhusiano kati ya mihimili hiyo unakuwepo, aliwaalika rais na spika wa bunge kuhudhuria siku ya kimataifa ya sheria. |
Subscribe to:
Posts (Atom)