Saturday, January 1, 2011

DAR HUYU NDO MFALME

NAKUBALI ETO'O ANASTAHILI UFALME WA SOKA AFRICA...


Kwangu mimi ni mmoja kati washambuliaji Hatari zaidi Duniani hasa anapolikaribia goli. Huyo ndio SAMUEL ETO'O FILLS wa Cameroon ambaye juzi aliweka Historia ya kuwa Mwanasoka pekee barani Africa kuweza kutwaa tuzo ya Mwanasoka bora barani humu kwa mara ya 4, maana kina GEORGE WEAH wa Liberia, ABEDI PELLE wa Ghana wamechukua mara 3 na ALHADJI DIOUF wa Senegal amechukua mara 2! ETO'O aliwapiku DIDIER DROGBA wa Ivory coast na ASAMOAH GYAN wa Ghana kwenye kuwania tuzo iyo. Ila najiuliza ivi ni kweli ETO'O ana miaka 29 na Drogba ana 32 kama inavyoelezwa au ni 'kanjanja' 2! Ebu fikiria eti NWANKO KANU ana miaka 34, wakati nimeanza kumsikia KANU tangu nasoma msingi na hata ukimwangalia usoni 2 utajua ana miaka zaidi ya 40 na kitu ivi daah, ama kweli Waafrica kwa mipango bwana...
BY KHADIL KANTANGAYO

No comments:

Post a Comment