Friday, August 5, 2011

LEO TUNAWARETEA MDUDU SISIMIZI

Sisimizi ni familia ya wadudu wadogo wanaoishi katika jamii. Jamii hizi zinaweza kuwa na sisimizi makumi kadhaa tu au kuwa na mamilioni kulingana na spishi mbalimbali.
Makazi yao yapo mara nyingi chini ya ardhi au mahali pengine panapohifadhiwa kama chini ya jiwe kubwa au katika nafasi ndani ya miti. Wanatumia udongo na nyuzi za mimea kwa ujenzi.
Jenasi kadhaa kama vile siafu (dorylus) hawana makazi ya kudumu bali wanahamahama.
Mchwa hawako karibu na sisimizi hata kama wanafana nao katika mengi na kuitwa kwa Kiingereza "white ants" lakini wako katika nasaba pamoja na kombamwiko.

Majina ya aina za sisimizi kwa Kiswahili



  • chungu (aina inayouma)
  • nyenyerere (wadogo weusi)
  • majimoto (aina nyekundu)
  • samesame (aina nyekundu)
  • sangara (aina nyekundu)
  • siafu (jenasi Dorylus)
  • sungusungu (aina kubwa nyeusi)